Mix

Kuhusu kumsajili Luis Suarez, Wenger asema haya.

on

339349_heroa

Meneja wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger amezungumzia kuhusu jaribio lake la kutaka kumsainisha mshambuliaji mtukutu mwenye kipaji cha  hali juu wa klabu ya Liverpool Suarez, na kusema hadhani kama atajaribu kutaka kumelta mshambuliaji huyo jijini London wakati wa dirisha la usajili litakapofunguliwa.

The Gunners walijaribu kumsaini mshambuliaji huyo wa Uruguay wakati wa dirisha la usajili la mwaka jana, huku Suarez mwenyewe akilazimisha kuondoka Anfield.

Lakini Wenger amezungumza na kusema hafikirii kama atatuma ofa nyingine kwa Liverpool kwa ajili ya Suarez.

“Uhamisho ulishindikana na hilo ndilo lilotokea. Hakuwahi kuw mchezaji wetu,” Wenger aliwaambia waandishi wa habari.

Baada ya kushindikana kwa uhamisho huo, Suarez alirudi na kusaini mkataba mpya na Liverpool, na mpaka sasa amesaidia timu hiyo kuwemo ndani ya TOP 4 akifunga mabao 23 katika mechi 19.

Arsenal inakutana na Liverpool katika dimba la Anfield jumamosi hii na wanaweza kuwazidi pointi 11 Liver ikiwa watashinda mechi hiyo, lakini Wenger anaamini kikosi cha Brendan Rodgers ambacho hakijafugwa kwenye mechi 7, kipo kwenye hali nzuri sana kufananisha na mara ya mwisho walipocheza Emirates ambapo Arsenal ilishinda 2-0.

Tupia Comments