Top Stories

Kuigawa Tanzania kwa Majimbo kutatugawa – JPM

on

“Mmesikia kwenye Kampeni za hivi karibuni mnaambiwa yatatengenezwa Majimbo,Tanzania itagawanywa ni Chama fulani kina sera yake hiyo ya kuigawanya Tanzania katika Majimbo ya Utawala, ukishatengeneza Majimbo katika Nchi huo ndio mwanzo wa mfarakano”

“Ukishagawanya Nchi katika Majimbo ni mwanzo wa ufarakano kwasababu kila Jimbo litakuwa linajitegemea lenyewe likiwa masikini linakuwa masikini wa kutupwa, Nyerere alipokuwa akiomba Uhuru wa Taifa hili angeligawa kwenye Majimbo tusingefikia hapa”

“Tanzania tuna Makabila zaidi ya 121, Nyerere alituweka Watanzania kama Taifa moja, tangu 1961 hatujaingia mfarakano kati ya Kabila na Kabila, Dini na Dini, Maeneo, sitaki nitoe mifano ya baadhi ya Nchi ambazo ziliingia kwenye mtego wa Majimbo na wamefarakana”

“Mngekuwa na Jimbo lenu hapa labda Jimbo la Tabora na wapi hizi Barabara tungetoa wapi hizo Bilioni 567, fedha hizi hazikutolewa na Tabora ni Tanzania nzima imeshiriki, Arusha, Mwanza, DSM wamechangia, kataeni mbinu za kutugawa kwa kusema watagawa Majimbo”

“Haya ya kuigawa Nchi kwenye Majimbo ni mambo wanayofundishwa huko wanakotoka na lengo ni kuifanya Nchi ivurugike ili wawe wanasomba kila kilichopo nchini, ukipigana na Mkeo hata Watoto hawana raha, sufuria unaweza kuikanyaga,tusikubali kutengenezewa Majimbo” <<< hayo ni maneno ya Mgombea Urais wa Tanzania kwa ticket ya CCM Dr. John Magufuli leo akiwa Urambo Tabora.

MTAZAME JPM LIVE KWA KUBONYEZA PLAY HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments