Top Stories

Ofisi nyingine za mawakili zavamiwa Dar es salaam (+video)

on

Siku chache baada ya ofisi za mawakili wa IMMMA kuvamiwa na watu wasiojulikana ambapo ililipuliwa na vitu vinavyodhaniwa kuwa ni mabomu, leo September 12 2017 tukio jingine lililohusisha ofisi ya mawakilili katika jengo la Prime House imevamiwa na watu wasiojulikana.

Inadaiwa kuwa watu takribani tisa walivamia jengo hilo lililopo Mtaa wa Tambaza Dar es salaam na kufanya uharibifu wa mali mbalimbali za wapangaji.

Jengo la Prime House lina ghorofa tano likijumuisha ofisi na kampuni mbalimbali ndani ikiwemo ofisi ya mawakili, duka la dawa na sehemu ya kufanya mazoezi ‘gym’.

Akizungumza na AyoTV na millardayo.com Wakili Asia Chali amesema mlinzi aliyekuwa zamu alimsimulia kuwa watu hao hawakuwa na silaha nyingine zaidi ya chuma na walienda ghorofa ya tatu ambapo kuna ofisi za mawakili hao na walivunja mlango na kuchukua baadhi ya nyaraka pamoja na kiasi cha shilingi milioni 3, Bonyeza play hapa chini kuitazama hii video hapa chini

Ulikosa hii ya mlinzi kusimuliwa kwa ofisi ya Wakili Fatma Karume, Bonyeza play hapa chini kutazama

Soma na hizi

Tupia Comments