Top Stories

Kuku amuua Mtoto wa miezi sita

on

Stori kutoka +254 Kenya katika eneo la Malava Jimbo la Kakamega zinasema kuku aliyemuua Mtoto wa miezi ameshambuliwa hadi kufa na Wanakijiji wa eneo hilo.

Inadaiwa kuwa mtoto huyo alifariki nyumbani kwao kwa mshtuko baada ya kushambuliwa na kuku ambaye alikuwa anajaribu kulinda vifaranga vyake.

Kulingana na ripoti iliyotolewa na tovuti ya The Standard, Mama wa mtoto huyo aitwaye Robai Toboko amesema, familia imebaki na majonzi kwa mtoto wake huyo wa miezi 6 kufariki akiwa mikononi mwake .

Nilikuwa nimempakata mwanangu, katika ile harakati yake kujaribu kumkamata mmoja wa vifaranga, kuku huyo alimrukia mtoto  kwa hasira na kumgonga usoni na bawa lake. Mtoto alishtuka na akaanza kulia kwa muda mrefu kisha akapoteza fahamu Mama wa mtoto

Aidha amesema mtoto wake alikuwa yupo vizuri kiafya ila alikata roho baada ya kupata mshtuko wa kushambuliwa na kuku, pia majirani walijitokeza kumsaidia japokuwa walikuwa wameshachelewa lakini walimuua kuku huyo pamoja na vifaranga vyake.

“TUMA HELA BABA YAKO AMEFARIKI, TUNUNUE SANDA” RAIS MAGUFULI

Soma na hizi

Tupia Comments