Marekani kupitia Ubalozi wake uliopo hapa Nchini imesema imetiwa moyo na hakikisho alilolitoa Rais Magufuli Januari 21, kuwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu utakuwa wa Haki na wenye uwazi.
Wamefurahishwa na mwaliko wa Rais kwa Waangalizi wa Uchaguzi wa Kimataifa huku wakitarajia uchaguzi ambao Wagombea na Raia wataweza kukutana kwa amani, walieleza mawazo yao na Kampeni zitakazofanyika kwa usawa.
Aidha, imetoa wito wa kuharakishwa kwa zoezi la uandikshwaji Wapiga Kura lenye uwazi, kuanzishwa kwa Tume Huru za Uchaguzi na kuteuliwa mapema kwa Waangalizi wa Uchaguzi wa Kitaifa na Kimataifa wa kuaminika.