Michezo

Kumbukumbu ya Birthday ya Marc Vivien Foe

on

Leo May 1 ni siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa ya kiungo wa zamani wa Timu ya Taifa ya Cameroon na Club ya West Ham United/Man City Marc Vivien Foe aliyefariki June 26 2003, kilichotokea katika uwanja wa Stade de Gerland, Lyon Ufaransa wakati wa nusu fainal ya FIFA Confederations Cup Kati ya Cameron vs Colombia.

Foe alipoteza maisha akiwa na miaka 28 kutokana na Cardiac Arest hii ni baada ya kuanguka ghafla Uwanjani na kupoteza maisha, Cardiac Arest ni hali ya ghafla ya moyo kuacha kufanya kazi na hutokea kutokana na matatizo ya kimfumo wa umeme katika misuli ya moyo na dalili kuu ya tatizo hili ni kupoteza fahamu.

Kabla ya dalili kuu kukufikia huwa kuna dalili viashiria ambazo ni, maumivu ya kifua upande wa kushoto, kuhisi kuzunguzungu na kujihisi kutaka kudondoka, kubanwa pumzi, na mapigo ya moyo kwenda kasi sana.

Credit @voh_updates

Soma na hizi

Tupia Comments