Kampuni ya Bima ya Jubilee leo imezindua kampeni yake mpya inayokwenda kwa jina la “There Is Living And There Is Living Free” ikiwa na maana kuna kuishi na kuishi huru.
Kampeni hiyo ina lengo la kuwafanya Watanzania wote kuishi huru na kuwa na amani ya moyo kwakuwa na Bima bora za maisha pamoja na bima za afya.
Kama tunavyofahamu uelewa wa masuala ya Bima hapa nchi ni chini ya asilimia 1, hivyo basi Kampeni hii ina lengo la kuongeza elimu na kueleza umuhimu wa matumizi ya Bima.