Top Stories

Kutana na mwanamke aliyepeleka pilipili China kwa mkoba na kufuata PHD (+video)

on

Bertha Mleke ambaye ni mhadhiri wa chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere aliyeamua kuwa mjasiriamali aliyeanzia kwenye kutengeneza pilipili na kuziuza hadi kupelekea kubeba kwenye mkoba na kusafiri nazo mpaka China kwaajili ya kutafuta soko.

Bertha ameelezea safari yake ya kwenda China ambako licha ya kupeleka pilipili pia ilimbidi afuate kujiendeleza kimasomo kwa kusomea PHD, ambayo imemfungulia milango ya kufanya bishara tofauti tofauti hadi kujikuta akifungua ofisi ya kuwaagizia mizigo watanzania China.

Pamoja na kufanikiwa hadi kuepelekea kupewa tuzo sita na wachina, bado Bertha hakuacha kutamani kufungua ofisi ya utengenezaji pilipili zake huko huko China licha ya kuwa changamoto kubwa ni kusafirisha aina ya pilipili zake za ‘mbilimbi’ anazotengenezea bidhaa yake.

….>>>”Nimeanza mbali sana kuanzia 2016 leo hii tunatimiza miaka mitano na tulianzia kwenye pilipili na baadae nikaanzisha biashara ambayo tulianzia kwenye stoo ndogo tu, wachina waliona tumeendelea wakatupatia tuzo, tuna tuzo kama sita, Nilivyoanza shule sijawahi kupumzika, watu walishangaa nasoma PHD huku nafanya haya”

VIDEO: 

VIDEO: PETER MSECHU ALIVYOMVISHA PETE YA NDOA MPENZI WAKE KANISANI

 

Soma na hizi

Tupia Comments