Ni Mrembo mwenye umri wa miaka 19 Zara Rutherford ambae time hii ameweka rekodi baada kuzunguka na ndege duniani akiwa peke yake ndani ya miezi mitano.
Safari yake ilitakiwa itumie miezi mitatu ila kwasababu ya changamoto alizopitia hususani hali ya hewa mbaya, ilimchukua muda mrefu zaidi.
Pamoja na kuwa mtu mwenye umri mdogo zaidi kukamilisha mzunguko huo, Rutherford ndiye rubani wa kwanza mwenye umri mdogo na Mbelgiji wa kwanza kuzunguka dunia akiwa peke yake kwenye ndege.
Kabla yake rubani wa kwanza mwanamke kuzunguka dunia alikuwa na miaka 30, Mmarekani Shaesta Waiz, hapo 2017.
Akiwa Veracruz, Mexico, alikumbwa na tetemeko la ardhi katika chumba chake cha hoteli, kwenye ghorofa ya sita.
“Ghafla jengo lilianza kuyumba sidhani kama nimewahi kushuka ngazi kwa kasi kiasi hicho, nilitarajia sehemu hatari zaidi ya safari hii iwe angani.” alisema.
Licha ya kukumbwa na changamoto mbalimbali, hakukata tamaa, aliendelea na safari yake mpaka aliporejea kwao Belgium.
Jitihada zote alizifanya kwasababu ya kuwatia moyo watoto wa kike, na pia kuwahamasisha kufuata fani za Sayansi, teknolojia, Uhandisi na Hisabati.