Jana January 26 kupitia msamalia mwema aliyekua akisafiri toka Shinyanga kuelekea Morogoro aliwasiliana na millardayo.com na kutoa taarifa kuhusu kuziba njia kwa madereva wa Malori eneo la Ziba wilaya ya Nzega Mkoa wa Tabora.
Sababu kubwa za madereva hao wa Malori kufunga barabara ni ile kauli yao waliyosema kuchoshwa na vitendo vya kutekwa na Majambazi kwenye eneo hilo,ambapo jana yake January 26 kulitokea kiotendo cha kutekwa kwa Madereva wa malori huku wakifanyiwa vitendo vya kinyama.
Miongoni mwa vitendo vya kinyama wanavyofanyiwa wanapotekwa ni pamoja na kupigwa na kuumizwa huku wakihusisha tukio la January 25 ambapo kuna mtu katobolewa macho,mwingine kakatwa masikio na mwingine kakatwa mguu.
Naomba nikuunganishe na hawa watu watatu walichokisema wa kwanza ni dereva aliyekuepo eneo hilo wa pili ni Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora Rpc Peter Charles na Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye ameteuliwa hivi karibuni Mh.Mathias Chikawe.
Msikilize Dereva kwa kubonyeza play.
Msikilize Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora[Rpc]Peter Charles kwa kubonyeza play.
Hii ni kauli ya Waziri wa Mambo ya ndani Mh.Mathias Chikawe bonyeza play kumsikiliza.