Top Stories

kutokea Uturuki wamekuja na taxi zitakazotumika baharini

on

Katika juhudi za kupunguza foleni katika Jiji la Istanbul Uturuki lenye Watu zaidi ya Milioni 16 na magari takribani Milioni 5, Istanbul City Lines wameamua kuleta Boti zitazofanya biashara ya Taxi.
Watu watakuwa wanatumia App maalum kujua Taxi ipi ipo karibu na eneo walilopo na kwa kuanzia zimetengenezwa Taxi (Boti) 45.

“Tutatengeneza Taxi nyingine zaidi ili zitumike kama School Bus kwa ajili ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na tayari Vyuo viwili vimeshatuma oda zao ila tunaangalia utendaji kazi wa hizi Taxi zilizopo kwanza kabla ya kutengeneza hizo School Bus” —— Sinem Dedetas, Mkuu wa Istanbul City Lines.

MAAGIZO YA WAZIRI MKUU MAJALIWA KWA VIONGOZI WA MIKOA NA HALMASHAURI

KWA MARA YA KWANZA KIKWETE KAFUNGUKA UTENDAJI KAZI WA RAIS SAMIA “MPAKA SASA ANAENDESHA NCHI VIZURI”

Tupia Comments