Premier Bet
TMDA Ad

Mix

Wanamgambo 30 wa Al-Shabaab wauwawa

on

alshababTaarifa kutoka 254 zinasema Jeshi la Kenya linalopambana na kundi la wanamgambo la al-Shabaab linasema mpaka sasa wapiganaji 30 wa kundi hilo wameuawa Kusini Magharibi mwa Somalia,Msemaji wa jeshi hilo Meja Emmanuel Chirchir ameelezea kuwa jeshi la Kenya lilishambulia kwa mabomu mojawapo ya kambi za kundi hilo katika eneo la Gedo Alhamisi Jioni.

Miongoni mwa waliofariki ni makamanda kadhaa wa kundi hilo,Al Shabaab mpaka sasa  hawajatoa tamko lolote kuhusu shambulizi hilo,kundi la Al Shabaab walikiri kufanya shambulizi la kigaidi mjini Nairobi mwaka jana dhidi ya jengo  la Westgate na kusemekana kuua watu 70.

Kenya imekuwa ikipambana na wapiganaji wa kundi hilo tangu mwaka 2011 Oktoba wanajeshi wake walipojiunga rasmi na vikosi vya muungano wa Afrika ambavyo tayari vilikuwa nchini Somalia kwa kazi hiyo.

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ameahidi kuwa majeshi ya Kenya yataendelea na vita dhidi ya wanamgambao hao tangu waliposhambulia Kenya mwaka jana.

Tupia Comments