Duniani

PICHA 3: Jamaa alipa kodi kwa mikokoteni mitano ya sarafu

on

Mfanyabiashara mmoja Marekani ambaye amezozana na idara ya magari nchini humo DMV ameamua kulipa kodi yake ya dola 3,000 sawa na Tsh mil 6.6 kwa kutumia mikokoteni mitano iliojaa sarafu 300,000.

Nick Stafford kutoka Cedar Buff, Virginia, aliwasilisha sarafu nyingi hatua iliolazimu mashine ya kuhesabu sarafu hiyo ya idara hiyo kushindwa kuzihesabu. Hatua hiyo inajiri kufuatia mgogoro kati yake kuhusu kuwasiliana na wafanyakazi kuwauliza kuhusu kodi yao.

Iliwalazimu wafanyakazi kutumia saa saba wakihesabu sarafu hizo hadi usiku. Walimaliza kazi hiyo ya kuhesabu mapema siku ya Alhamisi. Bwana Stafford aliambia BBC aliwasilisha pingamizi yake kwa sababu alizitaka idara za serikali kuangazia na kutoa majibu kwa maswala yanayowakumba raia.

Bwana Stafford ameelezea katika mtandao wake kwamba mgogoro wake na DMV ulizuka kwa sababu idara hiyo haikutaka kumpatia nambari za simu za moja kwa moja kuhusu afisa wa kuwasiliana naye ili kusajili magari matatu na kulipa ushuru kwa kuwa anamiliki nyumba tatu katika maeneo 3 tofauti.

Aliwasilisha ombi la kutaka kupewa nambari ya moja kwa moja kulingana na Bristol Herald Courier na akapewa nambari ya simu ambayo angepiga lakini alipoitumia aliambiwa kwamba haingeweza kuitumia kuuliza maswali.

Bwana Stafford alitaka kujua nambari hizo za moja kwa moja za maafisa wengine tisa ijapokuwa Idara hiyo tayari ilikuwa imeshughulikia swala lake na ombi lake lilipokataliwa alienda mahakamani kuwasilisha malalamiko yake.

Mapema wiki hii jaji mmoja alipinga maombi yake matatu aliyowasilisha, akikataa maombi alilowasilisha kwa DMV na wafanyakazi wake wapigwe faini. Hatahivyo wafanyakazi wa idara ya magari baadaye walimpatia nambari hizo alizotaka na tayari amezichapisha katika mtandao wake.

Bwana Stafford anasema kuwa idara ya magari ililazimika kukubali malipo yake kwa sababu sheria ya Marekani kuhusu sarafu mwaka 1965 inasema sarafu ni fedha halali na zinaweza kutumika kulipa madeni, kodi na mishahara.

Source: BBC

AyoTVMAGAZETI: Tuhuma za rushwa ajira 600 Dangote, Vigogo dawa za kulevya waja na mbinu mpya, Bonyeza play hapa chini 

Soma na hizi

Tupia Comments