Michezo

Kwa matokeo haya Man City wanahitaji jitihada kuikuta Liverpool

on

Game ya Liverpool dhidi ya Man City ndio game iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu katika uwanja wa Anfield, game hiyo hamasa yake ilikuwa ni ushindani wa kukaa kileleni kwa timu hizo ambazo kwa miaka hii miwili imekuwa ikichuana sana katika mbio za kuwania taji la EPL.

 

Man City leo wakiwa Anfield wameshindwa kupunguza tofauti ya point dhidi ya Liverpool kwa kujikuta wakipoteza kwa kufungwa magoli 3-1, huku kocha wao Pep Guardiola akilalamika kunyimwa penati mbili kutokana na Alexander Arnold kushika mpira mara mbili tofauti katika eneo la hatari.

Liverpool sasa wanaongoza Ligi kwa kuwa na point 34 wakati Man City wakiwa nafasi ya 4 kwa kuwa na point 25, huu ni ushindi wa 105 wa Liverpool dhidi ya Man City katika mashindano yote waliowahi kukutana, Man City ikishinda mara 56 na kutoka sare mara 53.

Magoli ya Liverpool katika mchezo huo wa 214 kwa timu hizo kukutana yalifungwa na Fabinho dakika ya 6, Mohamed Salah dakika ya 13 na Sadio Mane dakika ya 51 huku goli pekee la Man City likifungwa na Bernaldo Silva dakika ya 78.

Soma na hizi

Tupia Comments