Ripoti mpya Nchini Marekani imeonesha kuwa Wanaume wapatao milioni moja na laki tatu nchini humo wanafanya upasuaji wa kupunguza vitambi, matiti na kutengeneza six packs (plastic surgery) ili kupata muonekano wa kuvutia.
Wakati Wataalamu wa afya wakipaza sauti na kusema upasuaji wa aina hiyo sio sahihi kwa binadamu, ripoti hiyo imeeleza kuwa gharama za Wanaume hao kufanikisha hilo hufikia dola elfu nne kwa mwaka kwa kila mmoja ambazo ni zaidi ya shilingi milioni tisa pesa za kitanzania