Mwimbaji wa Nigeria aliyeshinda tuzo ya Grammy, Ayodeji Ibrahim Balogun, almaarufu Wizkid, ambaye hivi karibuni alitangaza kuachana na muziki, amefichua kazi yake inayofuata ambayo ni kuwa mwigizaji.
Wizkid alisema anataka kuwa mwigizaji kwa sababu anataka kubusu wanawake na kurushiana bunduki kwenye sinema na lifichua haya kupitia Instagram story yake hivi majuzi.
Aliandika kwa Pidgin, “Shebi I tell you I one in act film!…I just want dey kiss and shoot a gun for a movie. Daz all!!”!”
story hiyo ilikuja saa chache baada ya kuonekana akiwa na mtayarishaji filamu mahiri wa Nollywood, Kunle Afolayan.
Wakati huo huo, Wizkid pia amefichua kuwa anafikiria kuongeza muda wake wa mapumziko kutoka kwenye muziki.
Mwimbaji huyo wa ‘Essence’, ambaye awali alitangaza kuwa atakuwa nje ya studio kwa miaka mitatu au minne, alisema sasa anafikiria kuongeza muda wa mapumziko hadi miaka sita.
Wizkid aliandika, “Loving every bit of this holiday. naweza kudumu hadi miaka sita.”