Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli amesema Ndege ya Tanzania aina ya Bombardier Q400 iliyokuwa ikishikiliwa nchini Canada imeachiwa na itapokelewa jijini Mwanza hivi karibuni.
“Kwa taarifa tu, Ndege yetu iliyokuwa imeshikiliwa Canada imeachiwa, mtatangaziwa siku ya kuipokea na itapokelewa hapa Mwanza” – Rais Magufuli