Mix

Kwa watanzania wanaohitaji elimu ya pesa na biashara

on

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya K Finance LTD Judith Minzi ambaye kwa mara ya pili K Finance iliyo chini yake wameamua kukuletea mafunzo ya Ignite Business Clinic yatakayofanyika mwakani 2020 na ametoa wito kwa watu mbalimbali kujitokeza.

 

Mafunzo haya yataanza rasmi January 18 2020 Hekima Garden mada kuu ikiwa ni jinsi ya kutumia vipaji ili kufikia uhuru wa kiuchumi katika kuendesha maisha ya kila mtanzania ili kuondokana na uchumi tegemezi.

Hata hivyo mwenyekiti wa bodi ya K Finance Mama Devotha Minzi amewakaribisha watu mbalimbali kujitokeza katika Ignite Business Clinic kwani wao wamebobea katika mafunzo na utoaji wa mikopo pia.

“K finance imebobea katika mikopo lakini pia mafunzo ya kipesa na biashara, leo ningependa hasa kuzungumzia mafunzo kwa sababu mafunzo ni kitu muhimi sana kufanikisha hata ule mkopo mtu anauchukua ili ufanikiwe unahitaji kuwa na elimu ya fedha na kibiashara” alisema mama Devotha Minzi

Soma na hizi

Tupia Comments