Ni mmoja wa washambuliaji wanne wanaounda safu kali ya ushambuliaji ya klabu ya Manchester City ambayo mpaka sasa imeshafunga mabao zaidi ya 100 katika michuano inayoshiriki, Stevan Jovetic mshambuliaji wa kimataifa wa Montenegro aliyehamia City wakati dirisha kubwa la usajili wakati wa kiangazi.
Mshambuliaji ambaye pia alikuwa akiwindwa na Arsenal kabla ya kujiunga na City amefunguka na kusema alikataa kujiunga na Real Madrid kabla ya kukamilisha uhamisho wa £22m kwenda Eithad Stadium akitokea Fiorentina.
Pia amekiri kwaba angeweza kujiunga na City mapema zaidi mwaka juzi lakini aliamua kukaa msimu mwingine jijini Florence.
Jovetic alisema: “Pamoja na timu nyingine lakini vilevile Real Madrid walinitaka, lakini nilichagua Man City.
“Niliamua kuja hapa kwa sababu hii ni project kubwa yenye wachezaji wengi wazuri. Ilikuwa nije hapa mwaka mmoja uliopita, lakini nilikuwa na msimu mzuri na (Vincenzo) Montella na Fiorentina.”
Jovetic, ambaye alifunga mabao 40 katika michezo 134 games akiwa na Fiorentina, hajawa na msimu mzuri na City baada ya kukumbwa na majeruhi.