Mfuko wa hifadhi ya jamii kwa watumishi wa umma (PSSSF) kwa kipindi Cha miaka mitano wamefanikiwa kulipa madai ya kiasi Cha shilingi Trilioni 1.3 yaliyoathiriwa kutoka kwenye mifuko iliyounganishwa kwa wanufaika 10, 273 ambapo madai hayo yalilipwa ndani ya miaka miwili huku mfuko ukiendelea kulipa madai mapya
Aidha Mfuko huo umefanikiwa kuongeza thamani ya uwekezaji kwa 23.5% kutoka Trilioni 6.40 hadi Trilioni 7.92 ikiwa ni wastani wa ongezeko la asilimia 4 Kila mwaka.
Hayo aliyasema Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Hosea Kashimba wakati akizungumza na wahariri wa vyombo vya Habari kuhusu utekelezaji wa majukumu ya mfuko huo Toka kuanzishwa kwake Agosti 2018 Hadi Agosti 2023.
Alisema walifanikiwa pia kulipa kiasi Cha jumla ya shilingi Trilioni 8.88 kwa wanufaika 262,095 lakini pia kupata mapato yatokanayo na uwekezaji wa wastani 85 kwa mwaka
Pia Hosea alisema Thamani ya uwekezaji imeongezeka kwa asilimia 23.5 kutoka Trilioni 6.40 hadi Trilioni 7.92 sawa na ongezeko la wastani wa asilimia 4 kwa mwaka.
“Uwekezaji katika hati fungani za serikali (60% chini ya Kokomo Cha 100%), uwekezaji katika malengo, 15% chini ya kikomo Cha 30% kiwango Cha upangishaji huu ni 100% kwa majengo ya makazi na 72% kwa majengo ya kupangisha kwa ajili ya ofisi, matarajioni ni kufika 80% mwisho mwa mwaka huu wa fedha”
“Uwekezaji katika hisa za Makampuni (12% chini ya kikomo Cha 20%), uwekezaji katika Amana za mabenki (7% chini ya kikomo Cha 35%) na maeneo mengine (6%)
Kadhalika Hosea alisema serikali imelipa shilingi Bilioni 500 katika deni la shilingi Bilioni 731.4 la mikopo ya miradi ambayo mifuko iliyounganishwa iliikopesha serikali ili kutekeleza miradi ikiwemo ujenzi wa jengo la Bunge, chuo Cha serikali Cha Hombolo, Nelson Mandela Institute of Science and Technology na chuo kikuu Dodoma.
“Jambo la kulipa madeni ya serikali katika mfuko hususani lile la michango ya kabla ya mwaka 1999, lilichukua muda mrefu, takribani miaka 20, hata hivyo kupitia uongozi madhubuti wa serikali ya awamu ya sita “
Tangu kuanzishwa kwa mfuko huo, Mkurugenzi huyo alisema wamefanikiwa kulipa bila kukosa na kwa wakati pensheni ya Kila mwezi wastani wa shilingi Bilioni 67 kwa wastaafu Kila ifikapo tarehe 25 ya mwezi husika .
“Hili ni ongezeko la 100% ukilinganisha na kiasi Cha wastani wa shilingi Bilioni 34 wakati wa kuunganishwa”
Pia alisema wamefanikiwa kupunguza muda wa kusubiri mafao kwani mfuko unalipa ndani ya siku 60 kwa muhimu wa sheria.
Kuhusu uandikishaji wanachama, Hosea alisema PSSSF wamefanikiwa kuandikisha wanachama 140, 162 ambapo wengi wao ni waajiriwa wapua katika kada za afya, elimu na mashirika ya umma na Yale ambayo serikali Ina hisa zaidi ya 30%
Alisema idadi ya Wanachama kwenye mfuko kwa sasa ni 731,183 ME, na 296,516 KE.
“Pongezi kwa serikali kwa kuendelea kutoa ajira kwa watanzania ambao ndiyo nguzo muhimu katika kuendeleza mfuko huu”
Alisema PSSSF malengo yao ni kuboresha huduma kwa wanachama wa mfuko na kuwezesha mifuko ya pensheni kulipa mafao kwa mujibu wa mkataba wa ILO.
“Mfuko umeboresha huduma katika nyanja zote na kuwa na uwezo wa kutumia TEHAMA kwa asilimia 90 pia mfuko kwa sasa unalipa mafao kwa mujibu wa mkataba wa ILO”
Kwa upande wa Matarajio ya baadae ya mfuko huo, Hosea alisema wanatarajia kuwa karibu zaidi na wanachama wakati wote kuanzia wanapoajiriwa hadi wanapofikia muda wa kustaafu.
Pia Mfuko huo unatarajia kupunguza muda unaotumika kulipa mafao kutoka siku sitini za sasa hadi kufikia siku zisizozidi 30 lakini pia kuendelea kutoa elimu kwa wanachama na wadau mbalimbali ili kuongeza ufahamu wa huduma za mfuko na dhana nzima ya hifadhi ya jamii.
Pamoja na hayo, mfuko huo unatarajia kuingia mikataba na waajiri waliokuwa na malimbikizo ya michango pamoja na michango ya ziada iliyoathiriwa wengi wao wakiwa ni Halmashauri na hivyo kuathiri ulipwaji wa mafao kwa wakati, kwa sasa .
“Kwa sasa mikataba 78 imesainiwa kati ya Halmashauri 184, tunatarajia Hadi kufikia tarehe 30 septemba 2023 mikataba yote itakua imesainiwa”