AyoTV

VIDEO: Rais Magufuli alivyoamuru shule inayomilikiwa na CCM kuchukuliwa na Serikali

on

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo January 02 2017 amemaliza ziara yake ya siku mbili Mkoani Kagera kwa kuwatembelea baadhi ya wananchi walioathiriwa na tetemeko la ardhi pamoja na kukagua baadhi ya miundo mbinu iliyoathiriwa na tetemeko hilo na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa majengo ya shule ya sekondari ya Ihungo Omumwani iliyobomolewa na tetemeko la ardhi la Septemba 10,2016.

Mara baada ya ukaguzi huo Rais Dkt Magufuli akazungumza na wananchi wa Mkoa huo wa Kagera katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Ihungo.

Pamoja na mambo mengine  Rais Dkt Magufuli ameagiza shule ya Sekondari ya Omumwani iliyokuwa inamilikiwa na Jumuia ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi CCM imilikiwe na Serikali kutaka wanafunzi wote wanaosoma katika shule hiyo kutolipa ada kama zilivyo shule nyingine za serikali. Bonyeza Play hapa chini kutazama

VIDEO: ‘Hakuna mchango mwingine utakaoletwa ofisi ya waziri mkuu unaohusu Kagera’;-JPM, Bonyeza play hapa chini  kutazama 

unazitaka Breaking NEWS na Stori zote? ungana na Millard Ayo kwenye Facebook Twitter Instagram na Youtube na atakuletea matukio yote ya picha, video na habari iwe usiku au mchana…. bonyeza hapa >>> FB Twitter Instagram YouTUBE

Soma na hizi

Tupia Comments