AyoTV

VIDEO: Agizo lililotolewa kwa wakurugenzi nchini kuhusu maafisa uvuvi

on

Leo January 7 2017 kumefanyika kikao cha kamati kilichohusisha wizara saba za Maliasili, Ulinzi, Nishati na Madini TAMISEMI, Kilimo, Mifugo na uvuvi pamoja na Mambo ya Ndani ikiwa ni kikao hicho ni utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais la kupambana na uvuvi haramu.

Katika kikao hicho serikali imewaagiza wakurugenzi nchini hasa kwenye maeneo wanayojishughulisha na uvuvi kuwachukulia hatua maafisa uvuvi wanaoshindwa kutimiza wajibu kwa kushindwa kuzuia uvuvi haramu.

Naibu Waziri wa TAMISEMI Suleiman Jaffo aliwataka watendaji hao kutumia ajenda ya kupambana na uvuvi haramu kuwa ajenda ya kudumu  katika vikao vyao.

Kuna baadhi ya mafisa uvuvi wanahusika na vitendo vya uvuvi haramu nchini hivyo kuanzia kesho wataanza kupimwa wajibu wao na kwa atakayeshindwa kutimiza wajibu atatolewa katika nyazifa hiyo”.

Kwa upande wake Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Januari Makamba alisema kuwa >>>>nchi yetu ina maeneo kubwa la bahari na kwa miaka kadhaa nchi yetu imekuwa na changamoto ya uvuvi haramu, hivyo tumeona kuna haja ya kuchukua hatua ya haraka katika kupambana na uharamia huo.

Naye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba alitoa wito kwa watanzania wote kushirikiana na Serikali katika kufichua wale wanaohusika na uvuvi haramu. Unaweza kutazama video hii hapa chini.

VIDEO: Mashamba yaliyonyang’anywa kwa vigogo kupewa vijana kwa masharti, Bonyeza play hapa chini kutazama

Soma na hizi

Tupia Comments