Msichana wa miaka 14 wa Kenya ameshtakiwa kwa makosa kadhaa ya mauaji kwa kuwasha moto kwenye bweni la wanafunzi katika Shule ya Wasichana ya Moi, Nairobi na kusababisha vifo vya wanafunzi tisa.
Mtandao wa The Citizen umeripoti, kwa mujibu wa vyanzo ndani ya Mahakama ambako shauri hilo liliendeshwa kwenye camera kutokana na umri wa mtuhumiwa, msichana huyo alikana kuwasha moto September 2 uliochoma bweni la Moi Girls High School.
Vyanzo vya karibu na upelelezi vilidai kuwa, waligundua meseji kwenye group la WhatsApp kwenye simu ya mtuhumiwa ambapo alibainisha mipango yake ya kuchoma moto shule na moja ya meseji hiyo ilisomeka;>>>”Nitachoma moto shule.”
Indaiwa msichana huyo alikasirika kitendo cha wazazi wake kumpeleka Moi Girls, badala ya chaguo lake.
Miili ya wasichana waliofariki kwenye ajali hiyo haikuweza kutambuliwa haraka kutokana na kuungua sana mpaka vilipofanywa vipimo vya vinasaba ‘DNA’ vilivyokamilika Jumanne.
ULIPITWA? Nyumba 90 zachomwa moto, ni agizo la Mkuu wa Mkoa
TUJIKUMBUSHE! Vitu vya kukumbukwa kila September 11 Marekani