AyoTV

VIDEO: Ufafanuzi kuhusu taarifa za kukamatwa Watanzania wanaodaiwa ni majasusi Malawi

on

Baadhi ya vyombo vya habari vya hapa nchini hivi karibuni vilitoa taarifa kuwa, Watanzania 8 wanaodaiwa kuwa ni majasusi wa Serikali ya Tanzania wamekamatwa nchini Malawi kwa tuhuma za kuingia kwenye mgodi wa urani wa Kayerekera uliopo nchini Malawi kinyume cha sheria.

Taarifa hiyo kwa mara ya kwanza ilitolewa na chombo cha habari cha Malawi ambacho kilidai kuwa watu hao wametumwa na Serikali ya Tanzania ili kuchunguza kama Serikali ya Malawi inatengeneza silaha za nyuklia kwa kutumia madini ya urani ya kutoka mgodi huo.

Kufuatia taarifa hizo, Wizara ya mambo ya nje kupitia ubalozi wa Tanzania nchini Malawi ulifuatilia ili kubaini ukweli wa tukio hilo. Baada ya kufuatilia ilibainika kuwa ni kweli Watanzania 8 kutoka taasisi ya CARITAS iliyo chini ya Kanisa Katoliki Songea mkoani Ruvuma walikamatwa na vyombo vya usalama katika wilaya ya Karonga ambayo inapakana na Wilaya ya Kyela.

Watanzania hao mara moja walifunguliwa kesi kwa kutuhumiwa kufanya kosa la jinai la kuingia eneo la mgodi bila kibali (criminal trespass). Ubalozi unaendelea kufanya mawasiliano na Kanisa Katoliki Songea ili kupata maelezo zaidi kuhusu ziara ya watu hao kwa madhumuni ya kuyawasilisha mamlaka husika ili watuhumiwa waweze kutolewa.  Bonyeza play hapa chini kumsikiliza msemaji wa wizara ya mambo ya nje akifafanua zaidi

VIDEO: Msimamo wa TZ kuhusu mgogoro wa mpaka na Malawi kwenye ziwa Nyasa, Bonyeza play hapa chini 

Soma na hizi

Tupia Comments