Mix

AUDIO: Sababu za Waziri Mwakyembe kuagiza Nay wa mitego kuachiwa

on

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, ameliagiza Jeshi la Polisi kumuachia huru Msanii Ney wa Mitego ambaye alikuwa akishikiliwa na Jeshi hilo.

Waziri Mwakyembe ameishauri pia BASATA kuondoa zuio lake dhidi ya wimbo wa ‘WAPO’ na badala yake uendelee kupigwa tu kama nyimbo nyingine.

Akiongea na Wandishi wa Habari Dodoma, Dk. Mwakyembe amesema hata Rais Magufuli amefurahishwa na wimbo huo wa WAPO na kumshauri Msanii huyo kama inawezekana aendelee kutaja watu wengine kama vile wakwepa Kodi, wauza Unga, wanaotumia dawa za kulevya pamoja na watu wengine wasio na maadili mema katika jamii.

Unaweza kuendelea kumsikiliza Waziri Mwakyembe kwenye hii sauti hapa chini akieleza yote…

VIDEO: Agizo la Waziri Nchemba kwa Askari wanaobambikizia watu kesi 

BREAKING NEWS zote na stori za mastaa utazipata kwa Reporter wako MillardAyo, hakikisha umejiunga na mimi kwenye Facebook, Twitter, Instagram, Snapchat, Youtube, APP kwenye ANDROID na IOS kote huko kwa jina hilohilo la @millardayo

Soma na hizi

Tupia Comments