Michezo

La Liga: Matokeo ya FC Barcelona vs Sevilla na wafungaji

on

IMG_8985.PNG

Wakati wapinzani wao wa jadi Real Madrid wakizidi kuchanua kwenye uongozi wa ligi, FC Barcelona ambao hivi karibuni wamekuwa hawana matokeo ya kuvutia leo walikuwa uwanjani kuumana na Sevilla katika mfululizo wa mechi za ligi kuu ya Hispania – La Liga.

Wakiwa ugenini FC Barcelona leo wamefanikiwa kupata pointi 3 na ushindi mnono dhidi ya Sevilla.
Magoli matatu ya Lionel Messi, moja la Neymar na lingine Ivan Rakitic yameipa ushindi wa 5-1 vijana wa kocha Luis Enrique.

Messi alifunga magoli hayo katika dakika za 21, 72, na 78, wakati Neymar akifunga lake dakika ya 48 huku Rakitic ambaye ni mchezaji wa zamani wa Sevilla akifunga katika dakika ya 65.

Jordi Alba alijifunga katika dakika ya 47 na kuipa Sevilla goli la kufutia machozi.

Takwimu za Mechi
Barcelona: Bravo, Alves, Pique, Mathieu, Alba (Adriano 80), Busquets, Rakitic, Xavi (Rafinha 77), L Suarez (Pedro 74), Messi, Neymar.
Subs not used: Ter Stegen, Bartra, Sergi Roberto, Munir.
Booked: Mathieu.
Goals: Messi 21, 72, 78, Neymar 48, Rakitic 65.
Sevilla: Beto, Coke, Carrico, Pareja, Diogo, Krychowiak, Banega, D Suarez (Gameiro 62), Aleix Vidal (Deulofeu 62), Vitolo, Bacca (Aspas 74).
Subs not used: Sergio Rico, Reyes, Kolodziejczak, M’Bia.
Booked: Coke.
Goal: Alba OG 47.
Referee: Juan Martinez Munuera.
Attendance: 78,283

Tupia Comments