Habari za Mastaa

Baada ya kimya kingi Lady Gaga amerudi na style mpya kwenye ‘Til It Happens To You’! (Video).

on

Mara ya mwisho umesikia ngoma mpya kutoka kwa Lady Gaga ilikuwa ni lini mtu wangu!?… Baada ya ukimya wa muda mrefu hatimaye Lady Gaga amerudi kuchukua nafasi yake kwenye kurasa za burudani!

Najua tumezoea kuwa Lady Gaga ni mtu wa vituko sana, sio mavazi yake wala video zake za muziki… siku zote amekuwa mtu wa kufanya vitu vya kipekee zaidi ambavyo sio rahisi kwa wengi kuviiga vituko vya msanii huyo kwa asilimia mia.

gaga3

Time hii Lady Gaga amerudi tofauti kabisa na video ya wimbo wake mpya ‘Til It Happens To You’, video ambayo inabeba ujumbe mzito sana kwa jamii dhidi ya vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia, na kupitia page yake ya Twitter, Lady Gaga alipost tweet inayosema; >>> ” nimetengeneza wimbo huu kwa watu wote duniani wanaopitia wakati mgumu kwenye maisha yao.” <<< @ladygaga.

gaga

Hakuishia hapo, Lady Gaga alipost tena tweet nyingine na kusema… >>> “natumaini utafarijika na wimbo huu na kupata amani kidogo, kwani hauko peke yako kwenye hili”. <<< @laygaga.

gaga2

Kizuri zaidi kuhusu wimbo huu ni kwamba baadhi ya mapato yatakayopatikana kwenye faida ya mauzo ya wimbo huu yatatumika kufadhili taasisi mbali mbali zinazopambana na ‘vitendo dhidi ya unyanyasaji wa kijinsia’.

gaga4

Nimeisogeza video hiyo hapa chini, bonyeza play kuitazama.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi>>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata piausisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Soma na hizi

Tupia Comments