Duniani

Du!! Tazama maziwa 10 yanayotajwa kuwa na muonekano wa moyo duniani ..(+Pichaz)

on

Mtu wangu wa nguvu bado millardayo.com inakusogezea uzuri wa dunia, huenda umewahi kutembelea vivutio vingi vya utalii duniani lakini huenda hukuwahi kubahatika kufika wala kusikia kuhusu  maziwa haya mazuri ya kuvutia yenye muonekano wa umbo la moyo au kopa. Hii ni stori ambayo nimekutana nayo mtandaoni mtu wangu wa nguvu, hivyo nikaona sio vibaya September 22 nikakusogezea karibu yako Top 10 ya maziwa yenye muonekano wa moyo duniani. Chanzo cha hii stori ni World – World Top Top. Huu ni muonekano wake kwa juu

1- Ziwa Shimshal – Pakistan

heart_shaped_shimshal_lake_pakistan (1)

Hili ni ziwa lenye umbo la moyo na lipo katika bonde la Hunza Pakistan

2- Gaislacher See – Australia

gaislacher-see-lake

Hili lipo Australia katika mlima Gaislachkogel

3- Heart Lake – Canada

heart_lake_ompah_canada

Hili lipo Canada pembeni limezunguukwa na maua mazuri lipo karibu na Ompah, Ontario

4- The Coeur de Voh – New Caledonia

heart_shaped_coeur_de_voh_new_caledonia

Muonekano wake kwa juu umepambwa na maua yanayoelea juu ya maji.

5- Crater – Uturuki

heart_shaped_narlıgöl_lake_turkey

Crater lipo Uturuki mpakani mwa Cappadocia

6- Heart Lake – Urusi

heart_lake_peak_cherkogo_russia

Lipo Urusi na inatajwa kama unataka kuona muonekano wake kwa juu utatumia masaa 5 kupanda kilele cha mlima Cherskogo

7- Hili ni bwawa lipo USA (Marekani)

heart_shaped_lake_ohio

Bwawa hili pia lipo karibu na Strongsville Ohio

8- Chicago – Colorado – USA

chicago_lakes_mt_evans_colorado

Sio lazima ulitazame kwa juu ili ujue kama lina umbo la moyo hata kwa chini ukitazama Chicago linaonekana kuwa na umbo hilo.

9- Aral Sea – Kazakhstan

heart_shaped_aral_sea

Sehemu ya Kusini ya Aral Sea ndio inaonyesha muonekano wa umbo la moyo

10- Eros  – India

heart_shaped_eros_lake_chembra

Ukiwa unaelekea kilele cha mlima Chembra ni rahisi kuona muoneka wa Eros.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>YouTUBE

Tupia Comments