Michezo

Real Madrid yaibuka na ushindi mnono dhidi ya Sevilla, Ronaldo kapiga shuti nane, magoli je? (+Video)

on

Burudani ya soka la Hispania liliendelea usiku wa March 20, kwa michezo kupigwa ndani ya ardhi ya Hispania, Real Madrid ambao bado hawana matumaini ya kutwaa Ubingwa wa Ligi hiyo kutokana na kuzidiwa point kumi na wapinzani wao wa jadi FC Barcelona, wamecheza dhidi ya Sevilla.

Katika mchezo huo wa Real Madrid dhidi ya Sevilla katika dimba la Santiago Bernabeu ulikuwa unatoa nafasi kwa timu zote mbili kuibuka na ushindi, kutokana na takwimu za timu hizo, kwa mechi 5 za mwisho kabla ya mchezo wa leo Madrid alikuwa kafungwa na Sevilla mara mbili na kushinda mara matatu.

img_dduch_20160320-212958_imagenes_lv_propias_dduch_20160320-2-4-k75B-U40573223308yqE-992x558@LaVanguardia-Web

Real Madrid wakiwa na nyota wao Cristiano Ronaldo aliyeshinda goli moja dakika ya 64 na kukosa penati dakika ya 58 katika jumla ya mashuti yake sio chini ya nane aliyopiga langoni kwa Sevilla, wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 4-0.

Karim Benzema ndio alikuwa wa kwanza kupachika goli kwa Real Madrid dakika ya 6, Gareth Bale dakika ya 66 na Jese Rodriguez dakika ya 86, wakati Kevin Gameiro akiishia kukosa penati dakika ya 27, kwa upande wa Sevilla, kwa sasa Real Madrid imetimiza jumla ya 66 ipo nafasi ya tatu nyuma ya Atletico waliozidi point moja,

Magoli ya Real Madrid Vs Sevilla

https://youtu.be/4dGWp74b48U

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE

Tupia Comments