Michezo

Real Madrid waibuka na ushindi wa goli 10-2 dhidi ya Rayo Vallecano, Cheki Video ya magoli (+Pichaz)

on

Baada ya wapinzani wao wa jadi FC Barcelona kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 3-0 dhidi ya River Plate ya Argentina katika fainali ya Klabu Bingwa Dunia, Real Madrid wameamishia hasira zao katika mchezo wa Ligi Kuu Hispania dhidi ya klabu ya Rayo Vallecano.

fft104mm4068087

Real Madrid walikuwa katika dimba lao la nyumbani la Santiago Bernabeu huku timu yao ikiwa imesheheni mastaa wao kama Karim Benzema, Cristiano Ronaldo na Gareth Bale. Real Madrid wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 10-2 wakati Gareth Bale na Benzema wakiambulia kufunga hat-trick.

1450627582282_lc_galleryImage_The_referee_shows_a_red_c

Magoli ya Real Madrid yalianza kufungwa dakika ya 3 na DaniloGareth Bale dakika ya 25, 42, 61 na 70, Cristiano Ronaldo dakika ya 30 na 54 na Karim Benzema dakika ya 48, 80 na 90. Wakati magoli ya Rayo Vallecano yalifungwa na Antonio Amaya dakika ya 10 na Jozabed dakika ya 12.

Video ya magoli ya mechi ya Real Madrid Vs Rayo Vallecano

https://youtu.be/aoxVwov7g2E

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments