Michezo

Matokeo ya mechi ya Atletico Madrid Vs Real Madrid yapo hapa mtu wangu (+Pichaz&Video)

on

Baada ya klabu ya FC Barcelona kuchukua kipigo cha goli 2-1 kutoka kwa Sevilla siku ya Jumamosi ya October 3 katika uwanja wa Estadio R. Sanchez Pizjuan, wapinzani wao wa jadi Real Madrid waliingia dimbani Jumapili ya October 4 katika uwanja wa ugenini wa Estadio Vicente Calderon kucheza mechi na wapinzani wao kutoka mji mmoja wa Madrid.

1443987736-0cdb1865dbf9add2a5d0c615c6027de1

Real Madrid waliingia kucheza mechi dhidi ya wenyeji wao Atletico Madrid, kwa kawaida FC Barcelona na Real Madrid huwa wanapata upinzani mkubwa kutoka kwa Atletico Madrid kila mara wakutanapo, licha ya Real Madrid kuanza kwa kupachika goli la mapema kupitia kwa Karim Benzema dakika ya 9′ .

715

Goli ambalo halikuweza kuipatia ushindi na kuondoka na point 3 katika uwanja wa Estadio Vicente Calderon, kwani Atletico Madrid walikuja juu dakika ya 22 ya mchezo wakapata penati na Antoine Griezmann kukosa, ila hiyo ilikuwa kama chachu kwa Atletico Madrid kuendelea kutafuta nafasi, kwani kipindi cha pili dakika ya 83 Luciano Dario Vietto akaisawazishia Atletico Madrid na kufanya mechi kumalizika kwa sare ya goli 1-1.

1443988817-ba4199f12fa65013cdd49048c57af1b0

karim-benzema-atletico-madrid-real-madrid-la-liga_6ttak1gj3eup1ao075vgl2qbq

Hii ni video ya magoli mtu wangu

https://youtu.be/1BixQqc0yrg

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenyeTwitter,FB,Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAMTWITTERFBYOUTUBE

Tupia Comments