Michezo

Full Time ya El Clasico ya Real Madrid Vs FC Barcelona November 21 (+Pichaz&Video)

on

Ligi Kuu Hispania imeendelea tena leo November 21 kwa kuzikutanisha timu kadhaa kucheza mechi zao za muendelezo wa Ligi Kuu Hispania, miongoni mwa mechi zilizochezwa November 21 ni mchezo wa watani wa jadi kati ya Real Madrid dhidi ya mahasimu wao FC Barcelona katika dimba la Santiago Bernabeu jijini Madrid.

3334

Real Madrid na FC Barcelona kabla ya mchezo huu wa kihistoria kuchezwa walikuwa wamepishana kwa tofauti ya point tatu, Real Madrid wakiwa nyuma kwa kupoteza mchezo mmoja, huu ndio mchezo ambao kwa sasa una rekodi za kuangaliwa na watu wengi duniani. Licha ya kuwa Real Madrid wanaongoza kwa takwimu ya kumfunga FC Barcelona mara 92 kwa 89 hawakuweza kutamba katika uwanja wao wa nyumbani.

3600

Mchezo ulianza kwa FC Barcelona kupiga pasi nyingi kama kawaida yao na dakika ya 10 Luis Suarez akaanza kuwapa furaha mashabiki wa FC Barcelona duniani kote kwa kufunga goli la kwanza, wakati ambao Real Madrid wanajipanga namna ya kusawazisha goli hilo, Neymar akapachika goli la pili dakika ya 39 na kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa goli 2-0.

3137

Kipindi cha pili kilianza kwa FC Barcelona kuendelea kumiliki mpira hadi dakika ya 52 Andre Iniesta akapachika goli la tatu, FC Barcelona ambao dakika 4 baada ya Iniesta kufunga goli la tatu walimuingiza Lionel Messi kuchukua nafasi ya Ivan Rakitic ambaye alienda kuongeza nguvu na dakika ya 73 Luis Suarez akapachika goli la nne. Hadi dakika 90 zinamalizika FC Barcelona 4-0 Real Madrid.

Hii ni video ya magoli yote mtu wangu

https://youtu.be/qiRrdsy0K8I

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments