Michezo

FC Barcelona yaendeleza ubabe, Bilbao wamekutana na kipigo hiki (+Pichaz&Video)

on

Michezo ya Ligi Kuu Hispania imeendelea tena January 17 kwa michezo  kadhaa kupigwa katika viwanja mbalimbali nchini humo, wakati Real Madrid wakitembeza kichapo cha goli 5-1 dhidi ya Sporting Gijon , watani zao wa jadi klabu ya FC Barcelona imeendeleza rekodi ya kutoa dozi ya idadi kubwa ya magoli.

1453061360988_lc_galleryImage_Barcelona_s_Argentinian_f

FC Barcelona walicheza dhidi Athletic Bilbao usiku wa January 17 kuamkia January 18, wakati watani zao Real Madrid wakiondoka na point tatu na magoli matano dhidi ya Sporting Gijon katika mchezo wa mapema, hiyo ilikuwa kama ndimu kwa mchezo wa FC Barcelona uliochezwa usiku wa January 17, kwani walijibu mapigo kwa kuiadhibu Athletic Bilbao kwa jumla ya goli 6-0.

1453062691969_lc_galleryImage_Football_Soccer_Barcelona

Lionel Messi ndio alikuwa wa kwanza kupachika mpira nyavuni kwa mkwaju wa penati dakika ya 7 ya mchezo, Neymar dakika ya 31, Luis Suarez alifunga hat-trick dakika ya 47, 69 na 82 wakati Ivan Rakitic alipachika goli la nne dakika ya 62, kabla ya Luis Suarez hajafunga magoli magoli mawili ya mwisho. Kwa matokeo hayo FC Barcelona wenye point 45 wanakuwa nafasi ya pili nyuma ya Athletic Madrid aliyemzidi mchezo mmoja.

1453064698683_lc_galleryImage_Barcelona_s_Croatian_midf

Video ya magoli ya FC Barcelona Vs Athletic Bilbao

https://youtu.be/fHSM_tISaLA

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments