Michezo

Lamine Diack ahukumiwa miaka miwili jela

on

Mwanariadha wa zamani na Rais wa shirikisho la riadha Duniania (IAAF) Lamine Diack ,87, leo amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela Mahakamani nchini Ufaransa.

Diack aliyewahi kuwa Rais wa IAAF kwa miaka 16 (1999-2015) amehukumiwa kwenda jela baada ya Mahakama kujiridhisha kuwa alihusika na mpango wa kupokea rushwa na utakatishaji fedha kutoka kwa wanariadha wa Urusi aliowaruhusu kuendelea kushiriki mashindano licha ya kubainika kuwa walitumia dawa zisizoruhusiwa michezoni.

Lamine Diack ambaye ni raia wa Senegal adhabu hiyo imeambatana na faini ya euro 500,000/= (Tsh Bilioni 1.3)

Soma na hizi

Tupia Comments