Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imeruhusu Mabasi ya Mikoani yaanze safari saa tisa usiku ambapo imeagiza Wamiliki wa Mabasi wanaopenda kuanza safari muda huo wafike katika Ofisi za Mamlaka hiyo kuomba leseni na masharti ni lazima Madereva wasajiliwe ili kuwa na taarifa zao.
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa LATRA, Salum Pazzy ametoa kauli hiyo leo Dar es salaam akiwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa), Priscus Joseph.
Pazzy amesema LATRA inafanya kazi kwa kushirikisha na Wadau wakiwamo TABOA na hawana mvutano kuhusu muda wa kuanza safari za Mabasi kwenda Mikoani.
“Tunafanya kazi kwa kushirikiana, suala la kubadilisha ratiba za Mabasi awali muda ulikuwa ni yote lazima yaanze safari saa 12 asubuhi si zaidi ya hapo, lakini baadaye tuliruhusu ratiba zianze saa 11 asubuhi”
PLAY:”RUBANI KUGEUZA NDEGE, TARATIBU ZILIKIUKWA” TCAA YATOA TAMKO SAKATA LA NDEGE KUSHINDWA KUTUA DODOMA