Kabla ya kuamua kufanya matembezi kuitalii duniani, sio vibaya ukianza kwa kufanya tafiti mbalimbali kujiridhisha kuhusu mambo mbalimbali hasa sheria na taratibu zinazoongoza sehemu unazokusudia kuzitembelea.
Tunafahamu kila sehemu kuna sheria na taratibu zinazofuatwa, lakini zipo sehemu nyingine zina sheria na taratibu zinazoshangaza na kustaajabisha ambazo huwa hazipatikani sehemu nyingine duniani.
Leo May 4, 2017 nakuletea hizi sheria 5 ambazo zipo katika baadhi ya maeneo na huzikuti sehemu nyingine duniani zaidi ya hiyo.
1: Huruhusiwi kubadilisha bulb kama hauna leseni ya ufundi umeme – Victoria, Australia
Unaweza ukastaajabu, lakini swali la kujiuliza ni mechanics wangapi wanahitajika kubadilisha bulb katika mji wa Victoria? Jibu ni hakuna. Victoria ni mji wa pili kwa kuwa na watu wengi nchini Australia lakini ni kosa kubadilisha bulb kama hauna leseni ya ufundi umeme. Ukikamatwa kwa kosa hili unaweza kutozwa faini hadi Dollar 10 za nchini hiyo.
2: Ni lazima kutabasamu muda wote katika mji wa Milan, Italia
Sheria hii huenda ikawa ni rahisi kuitekeleza ingawa ina ugumu wake pia ambapo unaambiwa katika mji wa Milan nchini Italia ipo sheria ambayo huwataka watu kutabasamu muda wote, isipokuwa wakati wa msiba au unapotembelea hospitali.
3: Katika kila nyimbo tano zitakazopigwa radioni/TV mmoja lazima uwe wa msanii wa Canada
Moja ya sheria za Kamisheni ya Radio na Television Canada ‘CRTC’ ni kuzitaka radio na television za nchi hiyo katika kila nyimbo tano zitakazochezwa mmoja lazima uwe umeimbwa na mwanamuziki wa Canada.
4: Ni kosa kuwa mnene nchini Japan
Katika nchi ambayo imeutambulisha duniani mchezo wa sumo ni kosa kuwa mnene. Mwaka 2009, watunga sheria wameweka kiwango cha juu cha upana wa kiuno – hii inamaanisha kuwa kila mwanaume mwenye umri wa zaidi ya miaka 40 hatakiwi kuwa na kiuno chenye upana wa inchi 31 na wanawake wasizidi inchi 35.
5: Ni kosa kuflash choo baada ya saa 4 usiku Switzerland
Kuflash choo baada ya saa 4 usiku kwenye apartment ni kosa nchini Switzerland. Serikali ya nchi hiyo inalichukulia suala la kuflash choo ni kupiga kelele.
VIDEO: Ya kufahamu kwenye ripoti ya haki za binadamu Tanzania -2016. Bonyeza play kutazama…