Chama cha wanasheria Tanganyika (TLS) kinatarajia kufanya uchaguzi kumchagua Rais mpya wa chama hicho pamoja na Makamu Rais katika uchaguzi utakaofanyika April 14, 2018 ambapo kwa sasa Rais wao ni Mbunge wa Singida Mashariki (CHADEMA) Tundu Lissu ambae yupo katika matibabu Ubelgiji na jina lake halipo katika walioteuliwa kugombea.
Makamu wa Rais wa TLS amewataja wanaogombea na amezungumza sababu za jina la Lissu kutokuwepo Walioteuliwa kuwania nafasi hiyo na Kamati ya uchaguzi ya TLS ni Fatma Karume, Makamu wa Rais wa sasa, Godwin Ngwilimi, Godwin Mwapongo na Godfrey Wasonga.