Ni kwa zaidi ya wiki moja, jeshi la Israel limeendelea kuishambulia Lebanoni kwa mabomu, kwa lengo la kutokomeza Hezbollah.
Kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa uhasama, serikali ya Kiyahudi imeshambulia katikati mwa jiji la Beirut.
Jeshi la Israel limefanya mashambulizi siku ya Jumatatu, kwa mujibu wa chanzo cha usalama cha Lebanoni, katikati ya mji wa Beirut, kwa mara ya kwanza tangu kuzuka kwa uhasama kati ya Israel na Hezbollah mwaka mmoja uliopita. Takriban watu wanne wanaaminika kufariki.
Baada ya kifo cha kiongozi wake Hassan Nasrallah na viongozi wengine wa kundi hili la Kishia katika mashambulizi, Lebanoni, Syria na Iran zimetangaza siku kadhaa za maombolezo ya kitaifa, kuanzia Jumatatu Septemba 30.
Lebanoni, Syria na Iran zimetangaza siku kadhaa za maombolezo ya kitaifa baada ya kifo cha kiongozi wa Hezbollah Hassan Nasrallah aliyeuawa katika shambulio huko Beirut siku ya Ijumaa. Hezbollah pia imethibitisha kifo cha Kamanda Ali Karaké katika shambulio hilo.
Jeshi la Israel limetangaza kuwa limewaua “zaidi ya magaidi 20 wa vyeo tofauti” kutoka Hezbollah katika mashambulizi huko Beirut.