Nyota wa mpira wa vikapu nchini Marekani, LeBron James anasema anafikiria “kuondoka” kwenye mchezo huo baada ya timu yake, Los Angeles Lakers, kushindwa kufuzu kwa Fainali za NBA.
Lakers wanaoshika nafasi ya saba walitolewa na Denver Nuggets walioota kileleni katika Mchezo wa Nne wa mchujo wa NBA, ambao wao Nuggets walishinda 113-11.
James aliweka rekodi ya kibinafsi akiwa na pointi 31 katika kipindi cha kwanza cha Mchezo wa 4 Jumatatu usiku, na kuiongoza timu yake iliyofufuka hadi ukingoni mwa fainali, lakini akakosa mikwaju miwili ya kufunga katika dakika ya mwisho.
Akizungumza baada ya mechi ya mwisho ambayo ilikuwa msimu wake wa 20 wa NBA, ambapo alikua mfungaji bora wa muda wote wa ligi, alisema kampeni hiyo imekuwa “changamoto”.
“Sipati kichocheo cha kufanya mwonekano wa Fainali za Mkutano. Nimefanya, sana. Na haifurahishi kwangu kutoweza kuwa sehemu ya kufika Fainali,” alisema.
“Tutaona. Tutaona kitakachoendelea. Sijui. Nina mengi ya kufikiria kuwa mkweli. Nina mengi ya kufikiria kuwa mkweli. Kwangu mimi binafsi kwenda mbele na mchezo wa mpira wa vikapu, nina mengi ya kufikiria.”