Usiku wa October 18 2016 klabu ya Leicester City iliendeleza rekodi yao nzuri katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, hiyo ni baada ya kucheza mchezo wao wa tatu na kufanikiwa kukusanya jumla ya point zote 9 pasipo kuruhusu goli hata moja huku wakiwa wamefunga jumla ya goli 5.
Katika mchezo wa usiku wa October 18 dhidi ya FC Copenhagen, Leicester waliibuka na ushindi wa goli 1-0 lilifungwa na mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa PFA Riyad Mahrez ambaye pia ana mchango wa moja kwa moja katika kusaidia Leicester kufunga goli 4 kati ya 5 katika michuano hiyo.
Licha ya ushindi huo wa Leicester City katika uwanja wao wa King Power, imeripotiwa na BBC kuwa kufuatia kuwashwa kwa miale ya moto na shabiki wa Copenhagen kunaweza kufanya Leicester wakaadhibiwa na UEFA kutokana na kanuni.
Sheria za UEFA zinaeleza kuwa ulinzi wa uwanja kabla na wakati wa mchezo huwa ni chini ya uangalizi wa timu mwenyeji, kama Leicester itagundulika ulifanyika uzembe katika ulinzi basi inawezekana wakakumbana na adhabu kutoka UEFA.
ALL GOALS: Yanga vs Simba October 1 2016, Full Time 1-1