AyoTV

VIDEO: Diamond, RC Makonda, TSN na GSM walivyoguswa na kijana aliyetobolewa macho

on

Baada ya siku kadhaa tangu kutolewa kwa majibu ya madaktari juu ya uchunguzi wa Macho ya kijana Said maaarufu kama Baba D ambaye alipata mkasa wa kushambuliwa na mtu anayefahamika kwa jina la Scorpion, kisha kutobolewa macho yote mawili hali iliyopelekea kutoona.

Jitihada zilizofanywa na Serikali ya mkoa wa Dar es salaam zikiongozwa na mkuu wa mkoa Paul Makonda ili kuweza kumsaidia kijana huyo zilifanikiwa kumfikisha katika Hospitali ya Muhimbili ambako alifanyiwa uchunguzi wa kina ili kujua kama kuna uwezekano wowote wa kumrejeshea uwezo wa kuona, ripoti ya Madaktari ilionesha kwamba hakuna uwezekano wa aina yoyote ambao unaweza kumfanya kijana huyo kuona tena.

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Mkaonda aliahidi  Shilingi Milioni 10, na Leo kupitia kipindi cha Leo Tena cha  Clouds FM, RC Makonda ametimiza ahadi hiyo, Staa wa Bongo Fleva Diamond Platnumz nae alikuwepo kwenye kipindi hicho ambapo amemkabidhi milioni mbili, aidha kampuni ya GSM imeahidi kumnunulia nyumba eneo atakalolitaka Said Ally na pia kampuni ya TSN wametoa pikipiki mbili na wadau wengine wametoa pikipiki tatu na kufanya jumla ya pikipiki tano.

Unaweza kuangalia video hizi hapa chini

ULIKOSA HII YA PAUL MAKONDA AKITOA MAJIBU YA KIJANA ALIYETOBOLEWA MACHO BUGURUNI? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments