Bunge la 11 limeendelea tena Dodoma leo Mei 5 2016, Katika Kipindi cha Maswali ya papo kwa pako kwa Waziri Mkuu Mbunge wa Viti maalum (CHADEMA) Dr. Elly Marko Macha alimuuliza Waziri Mkuu Majaliwa..>>>
‘Tanzania ilisaini mkataba wa kimataifa wa mwaka 2006 kuhusu haki za watu wenye ulemavu, utaratibu ni kwamba baada ya miaka miwili baada ya kuridhia Serikali inataiwa kuwandika State Report, Kwanini Serikali haijapeleka hiyo ripoti hadi leo kuhusu watu wenye ulemavu?’
Waziri Mkuu Majaliwa akapata nafasi ya kujibu na kusema..>>>‘Serikali yetu imedhamilia kufungua milango na kutoa huduma na kuwafanya ndugu zetu wenye mahitaji maalum kuwa ni sehemu ya wachangiaji wakubwa wa shughuli za kimaendeleo nchini’
‘Mikataba hii baada ya kuwa tumeunda Serikali yetu tutafanya mapitio ya kazi zote za awamu ya nne ambazo zilikuwa zimefikiwa na tuweze kuunganisha mkakati ambao Rais ameuweka ikiwa ni pamoja na hili ambalo Dk. Macha umelieleza’
‘Nikuhakikishie, kwakuwa tayari tunaye Waziri mwenye dhamana ya Watu wenye mahitaji maalum basi wakati wowote kuanzia sasa jambo hili litakamilika na nimtake Dokta Abdallah Poss aanze mchakato wa kuwakusanya wadau wote ili tuanze kuyapitia mahitaji hayo‘
ULIIKOSA HII ‘WAMAMA AMBAO HAWABEBI MIMBA KUPATA UGONJWA WA MYOMA’ NAIBU WAZIRI KIGWANGALLA
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO‘ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa >>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE