Leo ni leo katika Ulimwengu wa soka ambapo ile michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya ngazi ya klabu (Yaani UEFA Champions League) inarejea kwa mechi mbili za kukata na shoka zitakazopigwa kwenye viwanja vya miji ya Paris nchini Ufaransa na Lisbon nchini Ureno.
Katika uwanja wa Le Parc des Princes jijini Paris, wenyeji PSG ambao hawajawahi kutwaa ubingwa watawakaribisha mabingwa mara 13 wa michuano hiyo Real Madrid kutoka Hispania, ambapo habari njema kwa PSG ni urejeo wa nyota wake Neymar ambaye amekosekana tangu mwezi Novemba 2021 kutokana na majeraha, jambo ambalo limethibitishwa na kocha wa timu hiyo Mauricio Pochettino alipozungumzia kikosi chake ambapo pia amethibitisha kuwa atamkosa beki mhisapnia Sergio Ramos ambaye ni majeruhi.
Kwa upande wake kocha wa Real Madrid Mzee Carlo Ancelotti, licha ya kukiri ugumu wa mechi hiyo ameeleza mpango aliouweka lakini pia akijivunia rekodi ya ya ushindi mara 3 sare 2 katika mechi sita ambazo timu yake imekutana na PSG.
Mechi nyingine itakayopigwa leo ni kati timu maarufu ambazo zote hazijawahi kushinda ubingwa wa michuano hii, ambapo wenyeji Sporting CP watawakaribisha Manchester City kutoka Uingereza kwenye uwanja wa Jose Alvalade jijini Lisbon, na kuelekea mechi hiyo kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema anatambua shinikizo lililopo la kumtaka ahakikishe timu hiyo inatwaa ubingwa na ameweka wazi kuwa huo ndiyo msimamo wake licha ya kuwa bado safari ni ndefu.
Pep amesema anajivunia uzoefu wa zaidi ya miaka 6 wa kikosi chake ambao amesema ni mtaji muhimu katika kusaka ubingwa ambao msimu uliopita aliukosa baada ya kufungwa kwenye mechi ya fainali na Chelsea.