Michezo

Rekodi 5 za Lewandowski ndani ya Bundesliga na kuingia katika kitabu cha Guinness World Records …

on

Mshambuliaji wa klabu ya FC Bayern Munich ya Ujerumani Robert Lewandowski ameingia katika headlines baada ya kuweka rekodi iliyoingia katika kitabu cha Guinness World RecordsRobert Lewandowski ambaye amekabidhiwa vyeti vyake na Guinness World Records baada ya kuweka rekodi hizo mwezi September katika mchezo dhidi ya Wolfsburg.

Robert-Lewandowski-secures-four-Guinness-World-Records

Rekodi aliyoiweka Lewandowski mwezi September dhidi ya Wolfsburg ya kufunga goli 5 za haraka akitokea benchi, huku timu yake ya FC Bayern Munich ikiwa nyuma kwa goli 1-0 lakini alivyoingia yeye ndani ya dakika 9 akafunga goli tano na kubadili matokeo kuwa ya 5-1. Imemfanya November 30 akiwa uwanja wa mazoezi wa Bayern amekabidhiwa vyeti vyake vya rekodi nne.

“Ulikuwa ni usiku wa kihistoria kwangu mimi, kwani ilinichukua siku na wiki nyingi kuweza kuweka rekodi hizi, familia yangu imefurahishwa na hili zaidi ya nilivyofurahia” >>> Lewandowski

Robert-Lewandowski-scores-five

Hata hivyo Lewandowski ana rekodi zilizoingia katika kitabu cha rekodi za dunia cha Guinness World Records ambazo ni rekodi ya kufunga hat-trick ya mapema Ligi Kuu Ujerumani, kuongoza kwa kufunga goli nne za mapema katika historia ya Ligi Kuu Ujerumani, mchezaji pekee aliyefunga magoli matano ya haraka Bundesliga na rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga goli nyingi akitokea benchi.
http://twitter.com/lewy_official/status/671356188450267136/photo/1

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyeza hapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Tupia Comments