Breaking News

BREAKING: Jamaa alienunua nyumba 3 za Bilioni 3 Lugumi leo DSM akamatwa na Polisi

on

Dakika kadhaa zilizopita zilianza kusambaa picha za Jamaa mmoja akiwa amevalia simple shati, tai suruali na sendoz chini na jina lake tukaambiwa ni Dr. Luis Shika na alionekana kwenye video akinunua kwa mnada nyumba 3 za Lugumi ambazo thamani yake ni zaidi ya BILIONI 3 Tsh.

Sasa taarifa za sasa ni kwamba Dr. Luis Shika amekamatwa na Polisi akiwa kwenye mnada huo na ni baada ya kudaiwa kuharibu mnada, imeelezwa ameshinda mnada wa kununua nyumba zote tatu lakini ameshindwa kutoa asilimia 25 ya malipo kama yalivyo masharti ya mnada hivyo mnada unarudiwa muda huu kwa watu wengine  huku yeye akiwa kachukuliwa na Polisi.

BUNGENI: Mbowe vs Waziri Mkuu Majaliwa… tazama hapa chini kwenye hii video

BREAKING NEWS: Hoteli ya Blue Pearl Ubungo yafungwa, Wageni waondolewa asubuhiasubuhi

UNAZITAKA BREAKING NEWS FASTAFASTA? Jiunge na Reporter wako Millard Ayo kwa kubonyeza kifuatacho SUBSCRIBE >>> YOUTUBE , APP YA MILLARD AYO, FACEBOOK , INSTAGRAM

Soma na hizi

Tupia Comments