Leo October 24, 2019 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Kangi Lugola amewataka Viongozi wa Jeshi la Polisi nchini kuhakikisha wanawatetea Askari wao wanaofanya kazi vizuri na kwa uwaadilifu wanaopata matatizo pindi wanapotekeleza majukumu yao .
Waziri Lugola amesema hayo Mkoani Dodoma wakati akifanya doria ya kubaini vitendo mbalimbali vya kihalifu vilivyokua vikifanyika Mkoani humo.
Akizungumza baada ya kufanya doria hiyo Waziri Lugola amesema Viongozi hao wanapaswa kuwatetea Askari wanaofanya kazi vizuri ya kupambana na wahalifu lakini baadhi yao wamekuwa wazembe na kutoa onyo kuwa askari yeyote atake uawa na jambazi atakua kafanya uzembe wa hali ya juu.