Michezo

PICHA 15: Dr Tulia na Naibu Waziri wa michezo walivyotoa burudani Mbeya leo

on

July 9, 2017 burudani ya sanaa na michezo ilikuwa Mbeya ambako Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura alizindua mashindano ya mpira wa miguu katika Wilaya ya Rungwe, Mbeya yaliyoandaliwa na Naibu Spika Dr. Tulia Ackson kupitia Taasisi yake ya Tulia Trust.

Huu ni muendelezo wa mashindano ambayo yamekuwa yakifanyika kila mwaka na time hii fainali ya mashindano hayo inatarakiwa kufanyika mwezi wa September.

Mbali na uzinduzi huo watu walishuhudia burudani ya ngoma za asili kutoka vikundi mbalimbali vya mkoani hapo na tayari nimekusogezea picha 15 nilizozinasa.

Baada ya uzinduzi michuano iliendelea

Dr Tulia aliposhiriki kucheza ngoma za asili

Kikundi cha ngoma za asili kikitoa burudani

Dr Tulia na watu wake wakiachia burudani ya ngoma za asili

Naibu Waziri Anastazia Wambura na Dr Tulia wakionesha moja ya jezi zitazotumika kwenye michuano

Dr Tulia na Naibu Waziri Wambura katika picha ya pamoja na baadhi ya wachezaji wa mpira wa kikapu

Dr Tulia akionesha ufundi wake katika mchezo wa mkono

Baadhi ya wachezaji wa mpira wa mkono wakiwa kazini

Naibu Waziri Wambura na Naibu Spika Dr Tulia wakisalimiana na baadhi ya wachezaji wa mpira wa mkono

VIDEO:Waziri Nape na Dk. Tulia walivyopanda kwenye stage moja kucheza ngoma za jadi 

Soma na hizi

Tupia Comments