AyoTV

Dr Tulia alivyomaliza mgogoro uliodumu kwa miaka mitatu Mbeya

on

March 10, 2018 Naibu Spika Dr Tulia Ackson alisafiri hadi katika kata Lufilyo Wilaya ya Busokelo mkoani Mbeya ambapo kulikuwa na mgogoro wa ujenzi wa zahanati na vituo vya afya uliodumu kwa zaidi ya miaka miwili mfululizo bila kupatiwa ufumbuzi.

Dr Tulia amesema “Leo tulikaa kwenye kikao na baadhi ya viongozi akiwemo Mkuu wa Wilaya pamoja na Mbunge na tumekubaliana kwamba Wananchi pamoja na viongozi mliotupa dhamana tutashirikiana pamoja nanyi kujenga vituo viwili vya afya” –Dr Tulia

Pamoja na hayo, vituo vya afya ambavyo tayari vimeanza kujengwa kwa nguvu za wananchi tumekubaliana kwa pamoja kushirikiana ili kuhakikisha tumevimaliza kwa pamoja. Lengo ni kuhakikisha tunaboresha miundombinu hii kwa ajili ya maslai yenu” –Dr Tulia

Alichokifanya Dr Tulia kwa watoto wenye ulemavu Mbeya

Soma na hizi

Tupia Comments