Mechi ya Nigeria ya kufuzu kwa Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Libya ilizama shakani baada ya kikosi cha Super Eagles kukwama usiku kucha katika uwanja wa ndege wa Al Abraq kabla ya kuruka nyumbani.
Wageni hao walipaswa kutua Benghazi Jumapili kabla ya mechi ya Jumanne ya kufuzu AFCON. Ndege yao ilielekezwa Al Abraq, takriban kilomita 230, ambapo majaribio ya kutatua hali hiyo hayakuzaa matunda.
Shirikisho la Soka la Nigeria limesisitiza kuwa kikosi hicho hakitasafiri kuelekea Benghazi kwa misingi ya usalama. Msemaji wa NFF aliiambia BBC Sport Africa kwamba timu yao ya taifa “imeachwa kabisa”.
Wachezaji akiwemo nahodha William Troost-Ekong na mshambuliaji Victor Boniface walisema wachezaji wa Nigeria waliachwa bila chakula wala maji kwa zaidi ya saa 12.
Meneja wa vyombo vya habari wa NFF, Promise Efoghe alilalamikia ukosefu wa mawasiliano au usaidizi kutoka kwa wenzao wa Libya, ingawa FA ya nchi mwenyeji ilikanusha madai kwamba mchezo mchafu unaendelea