Mamia ya wakaazi wa Derna nchini Libya, ulioathiriwa na mafuriko makubwa yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya Elfu tatu na kuwaacha maelfu bila makaazi, wameandamana, kulishtumu Bunge Mashariki mwa nchi hiyo na kutaka wale wote ambao hawakuajibika kuzuia janga hilo kuajibishwa.
Waandamanaji hao wametuhumu kiongozi wa bunge la eneo la mashariki Aguila Saleh,na mamlaka kwenye eneo hilo kwa kutowajibikia mafuriko hayo ambayo yamesababisha vifo vya karibia watu elfu nne kwa mujibu wa takwimu za umoja wa mataifa.
Katika taarifa ya pamoja, waandamanaji hao walisema wanataka uchunguzi wa haraka kufanyika kuhusu janaga hilo na sheria kuchukuliwa dhidi ya viongozi watepetevu.
Pia walidai fidia, uchunguzi juu ya fedha za jiji na ujenzi wa Derna.